Home  >  Submissions Your Words  >  SHAIRI-Shukrani kwa Mola
SHAIRI-Shukrani kwa Mola PDF Print E-mail
Your Words

Imeandikwa na Faith Anyango, Migosi Primary School, Kisumu, Kenya


Mimi mwana nainuka, kwa furaha ya kujaa

Asubuhi naamka, nashukuru jalia

Ninaoga kwa haraka, sare zangu kuzivaa

Shukrani kwako Mola, umenipa afya nzuri

 

Ninapofika mezani, chai nzuri i tayari

Inapofika tumboni, shuleni mbio safari

Mwalimu yu darasani, masomo kweli mazuri

Shukrani kwako Mola, umenipa afya nzuri

 

Nitasoma kwa bidii, niweze kuerevuka

Nisiwe mtoto bii, nisije kuharibika

Waalimu nitawatii, wazazi kuheshimika

Shukrani kwako Mola, umenipa afya nzuri

Imechorwa na Felix Paul Omondi