Home  >  Submissions Your Words  >  Shairi; Safari
Shairi; Safari PDF Print Email
Your Words

 

Kenya yetu ni bora

-Vivian Awour, Darasa la Nane (2012), Shule ya Msingi ya Lake, Kisumu


Kitenge nisiye shaka, natokea kiwanjani

Tumbo langu linawaka, kwa fikira za moyoni

 

Kila pembe nimesaka, nyikani na porini

 

Ndege ninamtafuta, wa kutulia tunduni

Moyo unanipapata, kwa kutembea porini

Ndege asiye matata, sijamwona asilani

 

Nimefika Githurai, nikaingia porini

Nikatega barawai, nikamnasa mtini

Kumbe ndege hafai, kahamia Kasarani

Nikaenda Rusinga, visiwa vyetu ziwani

Nikashika njiwamanga, nikafurahi moyoni

Siku mbili akaringa, kenda zake mafichoni

 

Nikenda tega Masaku, kwenye hewa milimani

Nikampata kasuku, mwenye sauti laini

Maneno kama chiruku, na uwongo mitaani

Najivunia kuwa Mkenya, Kenya yetu ni bora

 

-First published in Issue 10 2013.

FacebookTwitterGoogle BookmarksPinterest

safari